New American Alliance Ni Nini?
Karibu!
Mradi wa marejeleo ya New American Alliance unaunganisha wageni na rasilimali katika eneo la St.Louis na kwingineko. Tafuta orodha yetu kupata huduma za eneo au piga simu 314-655-0889 kwa usaidizi wa kibinafsi.
Jifunze

Kiingereza
Kuna madarasa mengi ya ESOL yanayopatikana katika mkoa wa St Louis ambayo husaidia watu wazima kujifunza Kiingereza katika viwango vingi.

Huduma za Afya
Tunatoa rasilimali ili kuruhusu watu binafsi kuchagua mhudumu wa afya bora anayepatikana ambaye anafaa zaidi na aliye bora kabisa.

Huduma za Kisheria
Tunatoa rasilimali ili kuruhusu watu binafsi kuchagua chaguo bora zaidi linalopatikana la kisheria kwa hali yao ya kipekee.
Tafuta katika Orodha
Tafuta katika orodha yetu ili upate rasilimali zinazopatikana St. Louis.Kwa maombi hususa au maswali, wasiliana nasi kwa 314-655-0889au kwa barua pepe kwa ballardj@iistl.org
English Lawyer Immigration Asylum Green Card Citizenship Doctor Job Business Hispanic LatinoWadhamini na Washirika

Kazi ya mradi wa marejeleo ya New American Alliance imewezeshwa na msaada wa ukarimu kutoka kwa Shirika la Afya la Missouri. Shirika hilo ni rasilimali kwa mkoa, linafanya kazi na jamii na mashirika yasiyo ya kibiashara ili kuanzisha na kuharakisha mabadiliko mazuri katika afya. Kama kichocheo cha mabadiliko, Shirika hilo linaboresha afya ya Wana Missouri kupitia ushirikiano, uzoefu, maarifa, na ufadhili.
New American Alliance ni ushirikiano kati ya Asian American Chamber of Commerce, Casa de Salud, Hispanic Chamber of Commerce, the International Institute, na Mradi wa Mosaic ya St. Louis Mosaic Project.